Geoffrey Lea wa Azam TV Arejea Clouds Media

Shaffi Dauda akimkabidhi mkataba Geoffrey Lea.

MCHAMBUZI wa soka nchini na basketball,  Geoffrey Lea, amerejea  kwenye kituo chake cha kazi cha awali, Clouds Media Group, ambako ametambulishwa rasmi na Meneja Vipindi wa Clouds, Shafii Dauda kwa kupatiwa mkataba wa kazi.

 

Yatuatayo ni maneno yaliyoandikwa kwenye mtandao wa Instagram wa Clouds kuhusu kurejea kwa mchambuzi huyo: Clouds wamethibitisha hilo kwenye mtandao wao wa Instagram, kwa kuandika, “#Breaking Usajili Mpya!
Kandarasi mpya ya mtangazaji @geoff_lea kuitumikia #CloudsMediaGroup karibu tena nyumbani Geofrey Lea tulichambue soka.”

Mtangazaji huyo anatarajiwa kurejea tena kwenye kipindi chake cha kuchambua michezo cha Sports Extra na vipindi vinginevyo.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment