The House of Favourite Newspapers

George Michael kituko sana!

0

michael

George Michael.

NEW YORK, Marekani

UNAMKUMBUKA George Michael, staa wa ngoma iliyokonga nyoyo za mashabiki kibao enzi zile ya Careless Whisper? Jamaa inasadikika yupo mbioni kurudi kwenye gemu baada ya kupotea kwa muda mrefu kutokana na kutopea kwenye madawa ya kulevya.

Kufuatia kupata huduma za ushauri nasaha, George Michael anarudi. Lakini ngoja tukukumbushe vituko vyake vilivyochangia aadimike kilingeni.

Aprili 1998, George alikamatwa na polisi akifanyiwa mchezo mchafu hadharani kwenye maegesho ya magari na baada ya hapo akautangazia ulimwengu kuwa yeye ni shoga.

Februari 2006 alikutwa na polisi akiwa ameanguka pembeni ya tairi la gari na alipopekuliwa akakutwa na bangi, miezi miwili baadaye alizigonga gari tatu zilizokuwa zimepaki, yeye akiwa na Range Rover.

Mei 2007, akakiri kosa la kukamatwa akiwa anaendesha gari wakati akijua kuwa amevuta madawa ya kulevya.

Septemba 2008, akaonywa kwa kupatikana na madawa ya kulevya aina ya cocaine na mengine.

Agosti 2010 akakiri kuendesha akiwa amevuta bangi na akafungiwa leseni kwa miezi sita.

Leave A Reply