George Mpole Apewa Mkono wa Kwaheri Geita Gold Mkataba wake Wamalizika
Uongozi wa klabu ya Geita Gold umethibitisha kuwa mkataba wake na kinara wa magoli Ligi kuu ya NBC msimu wa 2021/22, George Mpole umemalizika na kwamba makubaliano ya pande zote mbili yamefikiwa kuwa Mpole yupo huru kujiunga na klabu nyingine kuanzia leo Disemba 7 2022.
Geita Gold inamshukuru Mpole kwa kazi, ushirikiano na utendaji mzuri aliouonyesha kwa kipindi chote. Geita Gold inamtakia Mpole kila la kheri katika maisha yake ya mpira wa Miguu