The House of Favourite Newspapers

Georgina: Mimi Na Ronaldo Ni Wanandoa Machoni Pa Mungu… Adokeza Harusi Yao Hivi Karibuni

0
Georgina Rodriguez akiwa na mpenzi wake Cristiano Ronaldo

Georgina Rodriguez ametoa dokezo kubwa la harusi huku akidai yeye na Cristiano Ronaldo wamefunga ndoa mbele ya macho ya Mungu.
Inaaminika kuwa mwanamitindo huyo amekuwa akitoka kimapenzi na nyota huyo wa soka tangu mwaka 2016 na wanandoa hao wana watoto wawili pamoja.Mashabiki wamepata ufahamu wa kuvutia katika maisha yao katika siku za hivi karibuni kwa kutolewa kwa msimu wa pili wa Makala yake ya I Am Georgin inayopatikana kwenye Mtandao wa Netflix.
Huku kamera zikimfuatilia nyota huyo, alielezea uhusiano kati yake na Ronaldo kwa kina.
Alisema: “Kwa kweli nisingeweza kuolewa zaidi. Mimi na Cristiano tumefunga ndoa machoni pa Mungu, hilo ndilo jambo muhimu kwangu.””Anatulinda na kutuweka pamoja. Hata hivyo, siku moja sherehe itafuata. Nina bahati naweza kukuonesha ndoto kweli zinatimia. Ninathamini nafasi ambazo Mungu amenipa,” Aliongeza.


Georgina pia alifunguka juu yake kifo cha kuhuzunisha cha mmoja wa mapacha wake wakati wa kujifungua mwaka jana.Katika kionjo cha mfululizo huo, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 29 aliangua kilio akisema: “Maisha ni magumu, maisha yanaendelea. Nina sababu ya kuendelea na kuwa na nguvu. Cris alinitia moyo sana kuendelea na ahadi zangu zote.”Georgina amekuwa akijikaza kupata uzoefu wa maisha nchini Saudi Arabia katika miezi ya hivi karibuni.
Ronaldo amekuwa nyota wa Ligi Kuu ya Saudia katika klabu ya Al-Nassr tangu alipoondoka Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita.
Licha ya kuhama kwake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 anaendelea kuteka vichwa vya habari barani Ulaya na mapema wiki hii akiwa Ureno alivunja rekodi ya kucheza mechi nyingi za kimataifa na timu yake ya taifa hilo.

STORI NA SIFAEL PAUL

Leave A Reply