GF Automobile Ltd Yasaini Makubaliano ya Kimkakati Na NaCoNGO

Kampuni ya GF Trucks kupitia Kampuni ya GF Automobile imeingia makubaliano na Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini NaCoNGO (The National Council of NGOs).
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo, Mujtaba Karmali alisema katika makubaliano hayo yamelenga kunufaisha pande zote mbili wao kama wauzaji wa magari na mitambo waliona kuna haja ya kuingia makubaliano haya ya kimkakati kupitia mkataba huu ambao utafanya mambo mbalimbali ikiwamo kutoa elimu ya kuwajengea uwezo na uelewa katika nyaja mbalimbali.

Pia Karmali amesema wao wameanza mpango wa kuwapatia mafunzo kazi kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali mfano, VETA na DIT ili kuwajengea uwezo wa kuweza kufanya kazi na kupata uzoefu kazini.
Pia alisema makubaliano haya yatarahisisha kuwafikia makundi ya vijana nchi nzima na kuungana na serikali katika mpango wa kuhaikisha vijana wanajengewa uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri kwa kupita katika vyuo mbalimbali.
Nae Mwenyekiti wa NaCoNGO, Jasper Makala ameishukuru Kampuni ya GF Trucks kwa kuonyesha njia kwa makampuni ya Kitanzania kuchangia maendeleo ya Jamii kupitia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Alisisitiza kuwa ushirikiano na makampuni binafsi ya ndani ya nchi ni mbinu mojawapo ya kupunguza utegemezi toka nje ya nchi kuelekea katika uendelevu wa mashirika.