testiingg
The House of Favourite Newspapers

Gf  Trucks & Equiments Yatoa Msaada Kwa Vikosi Vya Jeshi La Uokoaji Kilimanjaro

0

Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deus akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vifaa kwa Afisa  mfawidhi daraja la kwanza na Kiongozi wa Geti ya Mweka   Denis Simion  wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya askari wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto katika mlima Kilimajaro.

 

 

Licha ya zoezi la uzimaji moto mlima Kilimanjaro kukamilika kwa asilimia 99 lakini vikosi mbali Vya jeshi la akiba  pamoja na askari wa wanyamapori bado wapo eneo la tukio kuzunguka mlima kwa ajili ya doria na kuhakikisha  masalia ya moto ulipo kwenye visiki wana udhibiti kwa haraka ili usilete madhara Zaidi.
  Akizungumza wakati wa kupokea misaada iliyotolewa na  kampuni  ya GF Trucks & Equipment’s Ltd  ,Kiongozi wa Geti ya Mweka Afisa Mfawidhi Daraja la kwanza Denis Simion  aliishukuru Kampuni ya GF kwa kuguswa na kupeleka misaada mbalimmbali ya vyakula kwa ajili ya askari hao wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto
“Unajua ndugu Mwandishi  moto ni  kama umedhibitiwa kwa asilimia 99 lakini hatuwezi viondoa vikosi vya askari wetu katika eneo la mlima kwani lolote lina weza kutokea kwa hiyo kuwa tayari kukabilianja na dharula inatakiwa askari wetu wawe doria muda wote” alimaliza Denis.
Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deus (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa askari   wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo
Naye Mkuu wa  kitengo cha masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF  Smart, Deus alisema kuwa wameguswa kutokana na ajali ya moto ya mlima Kilimanjaro  hivyo wakaamua kujikusanya na kutafuta utaratiobu wa kuja kukabidhi sehemu ya mchango wao kwa wapiganaji hao ambao bado wapo eneo tukio kwa ajili ya doria, miongoni wa vitu  ni pamoja na maji, soda mikate sukari na vingine vingi ikiwa nisehemu ya kurudisha kwa jamii faida waliyoipata katika biashara zao
GF Ni wauzaji wa magari ya FAW ,Hong Yang na mitambo aina ya XCMG pia kamuni hiyo inao utaratibu maalumu wa kuwakopesha magari na mitambo kwa wakandarasi wa kizalendo  wenye miradi mikubwa mkononi ilikukabiliana na ushindani na makampuni makubwa ya kigeni
Leave A Reply