The House of Favourite Newspapers

GGML Yatoa Milioni 100 Ujenzi wa Chuo Kikuu – Geita

0

KATIKA kukuza sekta ya elimu ya juu nchini, Kampuni ya Geita Gold Mining Ltd. (GGML) kupitia sera yake ya uwajibikaji kwa jamii imetoa kiasi cha Sh milioni 100 kusaidia ujenzi wa Kituo cha Chuo Kikuu Open University cha Mkoa wa Geita.

Awamu ya kwanza ya mradi huo inajumuisha ujenzi wa jengo la utawala linalojumuisha chumba mikutano cha viongozi, maktaba, chumba cha maabara ya kompyuta na ofisi nyingine tano.

Pia kiasi hicho cha pesa kilichotolewa na GGML ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi na malipo ya mafundi ujenzi.

Akizungumzia mradi huo, Makamu Rais – Maendeleo Endelevu katika kampuni hiyo, Simon Shayo alisema uwezeshaji huu unatarajiwa kufaidisha wanafunzi 500 wanaotokea katika vituo vitatu vya Mkoa wa Geita ambavyo ni Chato, Nyang’wale na Geita mjini.

Alisema GGML kwa kushirikiana na wananchi imeamua kuunga mkono juhudi za serikali kufadhili mradi huo kwani mbali na kuongeza mazingira bora ya upatikanaji wa elimu pia utazalisha wahitimu bora wenye weledi ndani ya jamii wataokuwa na uwezo wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa mbele kwa kupitia elimu waliyoipata.

NA MWANDISHI WETU

Leave A Reply