Ghasia za Capitol: Bunge la Uwakilishi Kumshtaki Trump

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema kwamba hotuba yake ya wiki iliyopita alipowataka wafuasi wake kuvamia bunge la Congress ‘ilistahili’.

 

Alisema kwamba ni upuuzi kwa wanachama wa Democrats kuweka juhudi za kumshataki bungeni kwa ‘kuchochea uasi’.

Anaondoka ofisini tarehe 20 Januari, 2021, wakati ambapo rais mteule, Joe Biden, ataapishwa.

 

Bunge la uwakilishi linatarajiwa kupigia kura kifungu cha sheria kuhusu kumshtaki rais huyo siku ya Jumtano.

 

”Nadhani mchakato huo wa kunishtaki unasababisha hatari kubwa kwa taifa letu na unasababisha hasira kubwa. Sitaki ghasia,”  Trump alisema.

 

Alikuwa akizungumza alipokuwa akiondoka katika Ikulu ya White House kuelekea jimbo la Texas ili kuchunguza sehemu moja ya ukuta uliojengwa katika mpaka wa taifa hilo na Mexico.

 

Ilikuwa mara ya kwanza kwa yeye kuonekana hadharani tangu ghasia za Capitol ambapo takriban watu watano walifariki na makumi kujeruhiwa wakiwemo maofisa wa polisi 60.

PRAYING for the PRESIDENT w/ FATHER FRANK PAVONE and the RSBN Team 1/12/21

Toa comment