The House of Favourite Newspapers

Giggy Money, Q Chillah wanaswa kimahaba!

IMG-20151128-WA0001Giggy Money akipozi kimahaba na Q Chillah.

KABAAANG!! Video Queen anayesumbua Bongo, Giggy Money hivi karibuni alinaswa na staa wa Bongo Fleva, Q Chillah wakiwa katika mapozi ya kimahaba ndani ya gari.

Chanzo kilicho karibu na Giggy kiliirushia picha hiyo Amani na kukipa ‘diteilz’ kuwa Giggy kwa sasa hashikiki wala haambiliki na staa huyo kwani wamekuwa wakiongozana kila wanapokwenda.

IMG-20151128-WA0017“Watakuwa ni wapenzi tu maana hata muda wa usiku wamekuwa wakionekana pamoja,” kilisema chanzo.

Amani lilimvutia waya Giggy kujua maneno hayo ambapo alisema kwa kifupi tu kuwa hawana uhusiano wowote wa kimapenzi zaidi ya urafiki na Chillah aliposomewa mashtaka hayo hakutoa ushirikiano.

Comments are closed.