The House of Favourite Newspapers

GIGY AFUNGUKA KUMWACHIA WEMA MWANAYE

MAMA bora! Msanii wa Bongo Flava mwenye mbwembwe na vituko lukuki, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefungukia ishu ya kumwacha mwanaye, Maira kwa Wema Isaac Sepetu kuwa, lengo ni ili amsaidie kulea kwani ni mama bora na mwenye upendo kwa watoto.

 

Akistorisha na Over Ze Weekend akiwa safarini jijini Mwanza huku akimwacha mwanaye kwa Wema jijini Dar, Gigy alisema amemuona Wema ana upendo na pia anapenda watoto hivyo akaamua kumuachia na kwenda kutafuta maisha akijua yupo mikono salama.

 

“Namuomba Mungu amjalie Wema apate mtoto maana ni mama mwenye upendo ndiyo maana nimemuachia Maira amlee na ninajua atakuwa kwenye mikono salama,” alisema Gigy akiwa kwenye ziara ya Tamasha la Wasafi Festival jijini Mwanza lililofanyika wikiendi iliyopita.

IMELDA MTEMA

Comments are closed.