The House of Favourite Newspapers

Gigy Awachefua Mashabiki

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ mapema wiki hii amewakera mashabiki zake mtandaoni baada ya kuposti video akiwa anaswaki na kutema mate hovyo, jambo lililofanya kila mmoja kuongea lake.

Mwanamama huyo asiyeishiwa vituko mjini, aliposti video hiyo na kuandika hivi “Mwenye kinyaa afe, ulitumwa? (Am savage and nasty) wee amekutuma nani?” aliandika Gigy.

Baada ya kuona hivyo, baadhi ya mashabiki zake walimjia juu na kila mtu kuongea lake ambapo kuna baadhi walisema anatakiwa ajiheshimu kwa sababu yeye ni kioo cha jamii na ni mama hivyo anapofanya vitu awe na mipaka.

“Jamani huyu dada hajiheshimu hata kidogo, sasa ndiyo nini kuonyesha huo uchafu wake hapa? Ndiyo maana Mo J alimuacha hata ningekuwa mimi nisingeweza kuvumilia ujiga huu, yaani anatia kinyaa,” alikomenti shabiki mmoja aliyefahamika kwa jina la @Maggie.

Leave A Reply