Gigy Money: 2020 kazi tu

MWANADADA machachari wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amesema mwaka huu amejipanga kuongeza juhudi katika kazi zake za muziki ili kujiongezea kipato hasa baada ya kuona matunda yake kwa mwaka 2019.

Akizungumza na Showbiz, Gigy alisema ni dhahiri kazi zake za kimuziki zimemuweka pazuri mpaka kufikia hatua ya kusaini mikataba ya kuwa balozi wa makampuni mbalimbali hapa nchini.

“Yaani kwa staili hii ya madili tu, basi naahidi ni kazi juu ya kazi kwani nimegundua kuwa hakuna kingine kinachoweza kukupa hela zaidi ya kazi nzuri ambazo zinakubalika na watu,” alisema Gigy

Stori: Ammar Masimba, Uwazi

Toa comment