Gigy Money Adaiwa Kunasa Kibendi

Gigy Money.

MUUZA ‘nyago’ na msanii wa filamu Bongo, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kubeba ujauzito wa mwandani wake Moulad Alpha ‘Moj’ ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Choice FM, ambapo za chini ya kapeti zinaeleza anafanya siri ili kuepuka kile anachokiita “kupigwa juju”.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, msanii huyo kwa sasa ana kibendi kipatacho miezi miwili ila amekuwa akihofia kueka wazi suala hilo sababu ya kuogopa kufanyiwa mambo ya kishirikina, ila watu wake wa karibu wengi wameanza kumstukia kutokana na dalili za wazi alizonazo.

Alipovutiwa waya na paparazi wetu kuhusiana na ishu hiyo alionekana kuuma maneno na kusema kuwa; “Sina mimba ila siku hizi nakula sana labda ndio maana watu wanahisi nina kibendi, pia siku hizi nimepungua mwili kwa sababu sifanyi tena mazoezi.

MAGAZETI: Mama Mobeto Amfyatukia Zari!

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment