GIGY MONEY ADAIWA KUNASA UJAUZITO

WAKATI mtoto wake, Mayra akiwa bado hajatimiza hata mwaka, msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni muuza nyago ‘video vixen’ Gift Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kunasa tena mimba. 

 

Kwa mujibu wa chanzo, Gigy ambaye alikuwa na uhusiano na mtangazaji Mourad Alfa ‘Moj’ na kuzaa naye Mayra, kwa sasa anadaiwa kunasa ujauzito wa mwanaume kutoka Nigeria.

 

“Gigy amenasa ujauzito na miezi kama miwili au mitatu na wala siyo ya Moj bali ya Mnigeria ambaye anaongozana naye kila kona na hata kwenye mitandao anamuanika,” kilisema chanzo.

 

Za Motomoto ilimtafuta Gigy kujua ukweli wa mimba hiyo ambapo alisema; “Mnataka kujua inawahusu nini? Haya mimba ninayo hiyo kusema ina miezi mingapi itawasaidia nini? Jueni kwamba ninayo tena ni ya Mnigeria wal a siyo Moj.”

 Na Shamuma Awadhi

Toa comment