Gigy Money amshika uchawi Amber Lulu

gigy-money-3Gigy Money

Stori: Imelda Mtema |Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Toleo la Jan 7, 2017

VIDEO Queen matata Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameanza mwaka mpya kwa kushusha madai makali kuwa Video Queen mwenzake Lulu Euggen ‘Amber Lulu’, anamroga na anaishi kwa kutumia nyota yake.

Akizungumza na gazeti hili Gigy alisema kuwa kuna vitu vingi sana amekuwa akifanyiwa na mrembo huyo kitu ambacho alikivumilia muda mrefu hivyo kwa sasa ameona ni bora kuviweka wazi.

amber-luluAmber Lulu

“Unajua Lulu, mimi nilikuwa nampenda sana kama ndugu yangu kabisa lakini naona vitu vyangu vingi haviko sawa ukifuatilia kwa wataalam unaambiwa ni yeye (Amber),” alisema Gigy.

Alipoulizwa Amber kuhusu tuhuma hizo, alisema: “Sijamroga yule, ana kipi? Aseme tu nimemzidi maarifa na kujitambua.”

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment