Gigy Money Amvaa Shabiki Kisa Kuhojiwa

MSANII wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amemcharukia vibaya mmoja wa mashabiki wake aliyehoji kuhusu ukimya wake kwenye muziki.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, juzikati msanii huyo aliwataka mashabiki wake wamuulize maswali akiwa hewani (live) na ndipo shabiki huyo alipomuuliza ‘kazi mpya lini?’ swali ambalo lilimchefua.

 

“Nahitaji muda wa kupumzika, watu wamenijua kabla ya kuanza kujiingiza kwenye muziki, kwa nini kuulizauliza hivi? Ndiyo maana Vanessa Mdee aliwahi kusema ‘muziki ni kitu ambacho kinachoweza kukufanya uishi maisha ya shida sana’,” alisema Gigy.

 

Gigy aliendelea kutoa povu juu ya mashabiki wanaodai kuwa yeye hatoi nyimbo, akiwasihi wamuache aishi anavyotaka na mtoto wake.

MAKALA: JOYCE NTITU NA SUSAN MANYAULI (TUDARCO)

WABUNGE Viti Maalum WAPIGA MAGOTI kumuombea MAGUFULI KURA, Hakuna KULALA Mpaka KIELEWEKE…
Toa comment