The House of Favourite Newspapers

GIGY MONEY, Unataka Mwanao Ajifunze Nini Kutoka Kwako?

Gift Stanford ‘Gigy Money’

KAMA wewe ni mfuatiliaji wa habari za wasanii Bongo, utakuwa unajua nini kinachoen­delea kwenye mitandao ya kijamii kati ya mwanadada Gift Stanford ‘Gigy Money’ na mwanaume ali­yekuwa akiishi naye, Moj.

Kama hujui basi siyo kesi, kwa ki­fupi ni kwamba Gigy Money, mwa­nadada ambaye ni video queen na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, yupo kwenye ‘mgogoro’ mzito na mpenzi wake, Moj, kiasi cha kufikia wawili hao ‘kuvuana nguo’ hadha­rani, ikiwa ni siku chache tu tangu Gigy ajifungue.

Gigy Money analalamika kwamba mwanaume huyo ambaye ni mtangazaji na wameishi pamoja kwa muda mrefu, amekuwa akim­nyanyasa kwa kumpiga, kumtolea lugha chafu na kwamba wakati mwingine amekuwa akimshindisha na njaa, kuanzia kipindi akiwa na ujauzito mpaka sasa baada ya kujifungua.

Kubwa ni kwamba Gigy anadai jamaa amekomba kila kitu kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja, na kumuachia ‘kagodoro’ na TV bila kujali kwamba mwen­zake ana mtoto mchanga.

Gigy akaenda mbali zaidi kwa kudai kwamba japokuwa alikuwa akiishi na Moj na hata siku anaji­fungua alikuwa naye, lakini ukweli ni kwamba yeye siyo baba halali wa mtoto bali kuna ‘njemba’ nyingine.

Moj naye kwa upande wake, amefunguka mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukanusha tuhuma zi­lizotolewa na Gigy, lakini ukitazama maelezo ya wote wawili kwa jicho la tatu, utagundua kwamba kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia. Kimsingi kama lawama alizozi­

toa Gigy Money ni za kweli, basi mwanaume atakuwa na makosa makubwa, tena sana. Niweke wazi kwamba masuala ya unyanyasaji wa wanawake, ni jambo linalopaswa kupingwa na kila mtu aliyestaarabika.

Pia mwanamke anapokuwa mjamzito au anapojifungua, anastahili kuoneshwa mapenzi ya hali ya juu, hata kama anakuwa na kasoro zake, hiki ni kipindi ambacho watu wote wanaomzunguka wanapaswa kumuelewa na kumvumilia, kwa hiyo kama ni kweli Moj ulikuwa unamdunda akiwa mjamzito na umshindisha na njaa, umefanya makosa makubwa.

Na kama kweli Gig Monye hayo uliyoyaeleza kweli yame­kutokea, nakupa pole sana. Hata hivyo, ukimfuatilia kwa karibu Gigy Money, inaonesha kwamba yawezekana kwa mara nyingine ameamua kutafuta ‘kiki’. Unaweza kushangaa kwa nini nimesema hivi lakini histo­ria inamhukumu Gigy, amekuwa na kawaida ya kutafuta kiki za ajabu-ajabu.

Sitaku kukumbushia ma­tukio yake, lakini nasisitiza inawezekana kabisa anachoki­fanya Gigy Money kikawa ni mwendelezo wake wa kiki.

Hata kama siyo kiki, ukifua­tilia maelezo yake anayoyatoa, anasema Moj siyo baba halisi wa mtoto na anamtaja mwa­naume mwingine, wakati huo­huo Moj naye anasema huyo mwanaume anaibiwa ukweli ni kwamba mtoto ni wake.

Yawezekana leo mtoto akawa hana uwezo wa kuelewa kinachoendelea lakini miaka kadhaa baadaye, akija kuwa na akili timamu, atajisikiaje kwa huu udhalilishaji anaofanyiwa na mama yake aliyembeba miezi tisa tumboni?

Sikia Gigy, umeshafanya drama nyingi sana ukiwa mwenyewe, lakini lazima ujita­mbue kwamba hivi sasa wewe siyo Gigy Money yule, wewe ni mama, ambaye mwanao ana­kutegemea kwa kila kitu, hebu acha mambo ya kitoto.

By the way umewahi kusi­kia wapi matatizo ya ndani yakamalizwa kwenye media? Kwani huna wazazi wewe? Huna ndugu au watu unaowa­heshimu unaoweza kuwatumia kuweka sawa mambo badala ya kufaidisha watu kwenye mitandao?

Acha hizo!

Comments are closed.