Gigy: Ukweli Wangu Nafukuza Wanafiki

MREMBO anayetamba kwenye muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema mara nyingi huwa anapenda kuwa mkweli hasa linapokuja suala la haki, ndiyo maana asilimia kubwa ya watu wanamuona hafai.

 

Akizungumza na AMANI, mwanamama huyo alisema kwamba, hawezi kuongea uongo kwa sababu amekua katika mazingira ya kuwa mkweli, ndiyo maana mara nyingi marafiki wasiofaa huwa wanamkimbia.

 

“Jamani mimi napenda kuwa mkweli, ukizingua nakupa makavu sikuachi wala nini, sasa kuna watu ambao wanapenda kila siku waambiwe wamepatia hata kama wamekosea.

 

“Ukiwaambia ili wajirekebishe, wanaanza kukusema vibaya, mwisho wa siku wanajitenga na wewe, mimi hilo sijali tena hao huwa nawaita wanafki, hata wakiondoka hawanipunguzii kitu,” alisema.

Stori: Memorise RichardTecno


Toa comment