The House of Favourite Newspapers

GLOBAL COLLEGES BASH KUWAUNGANISHA WASOMI NCHINI (VIDEO)

0
Washiriki wakishindana kukuna nazi.


TAMASHA lijulikanalo kama Global Colleges Bash linaloendelea sasa nchini  limelenga kuwaunganisha wasomi katika vyuo kwa lengo la kuhamasishana  katika masomo na michezo.

Watazamaji wakishuhudia.

Tamasha hilo ambalo limeanza kadiri ya mwezi mmoja uliopita na linaendelea katika mikoa mbalimbali linahusisha riadha, kukimbiza kuku, kula ugali bila mboga, soka, red carpet,  nguo za ‘zilipendwa’, kula mkate kwa dakika tano, kushindana kucheza muziki, kuogelea na michezo mingine mingi ambayo itawakutanisha wasomi hao na kubadilishana mawazo.

 Global Colleges Bash ikiendelea.


Hata hivyo,  wanafunzi wanaoshiriki katika tamasha hilo ni hususani wale wanaochukua masomo ya uandishi wa habari, japokuwa na wengine wanaruhusiwa kushiriki.

College Bash inadhaminiwa na wafadhili mbalimbali, ambapo tangu mwanzoni wafadhili waliojitokeza ni kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Global Publishers Ltd. Global TV Online ndiyo wafuatiliaji na watangazaji wakuu wa tamasha hilo.

Wanafunzi wa vyuo wanaotaka kushiriki katika burudani hiyo ambayo inaendelea hadi mikoa mbalimbali nchini bado wana fursa ya kujitokeza na kuungana na wenzao.

NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Leave A Reply