Global Digital Yatangaza Mafuzo na Ajira kwa Vijana

 

GLOBAL DIGITAL LIMITED

Maendeleo ya Sayansi na Technolojia yanaendelea kutengeneza fursa kila siku kwa vijana wa kike na kiume wenye kuitumia vizuri kwa kujiingizia kipato halali, hasa kwa upande wa mitandao ya kijamii. kwa kulitambua hilo, Kampuni ya Global Digital imetoa fursa ya Mafuzo na Ajira kwa vijana wenye mapenzi na kazi za mitandao ya kijamii,  wanaopenda kufuatilia Habari, Burudani na Maisha ya wasanii mitandaoni.

 

Inazo nafasi kadhaa kwenye upande wa mtandao wa You Tube, zitakazotolewa kwa vijana wenye mapenzi (Hobbies) ya kufuatilia mtandao huu, ambao watapewa mafunzo ya miezi miwili yatakayowawezesha kuelewa kiutaalamu zaidi mtandao huo unavyofanyakazi na unavyoweza kubadilisha maisha ya mtu, kielimu, kiuchumi na kijamii. Vijana watakaofaulu vizuri mafunzo hayo, watapewa ajira ya kudumu katika kampuni.

 

VIGEZO NA MASHARTI

Kijana anayetafutwa awe na vigezo na sifa zifuatazo:

Awe na Elimu wa Sekondari au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ya Tanzania

Awe na Uwezo wa kuandika na kuongea kwa ufasaha lugha za Kiswahili na Kiingereza

Awe anamiliki na kujua kutumia zuri simu janja (Smart Phone)

Awe anayefuatilia kila siku mtandao wa You Tube

Awe anapenda burudani na kufuatilia habari za kila siku mitandaoni

Awe na umri usiozidi miaka 25 na asiwe chini ya umri wa miaka 18

awe kijana wa kiume aishie jijini  Dar es salaam

Miwsho; awe anaishi maeneo ya Sinza, Mwenge, Kijitonyama au Kinondoni.

Kama Unazo sifa hizo, tafadhali tuma maombi yako ukiambatanisha na vyeti vyako kwa:

KOZI YA YOU TUBE

GLOBAL DIGITAL LIMITED

email:globaldigital255@gmail.com

SINZA MORI, MORI ROAD

DAR ES SALAAM

SIMU: 0655 919932


Loading...

Toa comment