Global FC kuichakaza DSJ leo

MATAJIRI wa Sinza, timu ya Global FC, leo Ijumaa wanatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji cha Dar es Salaam (DSJ) kwenye Uwanja wa Boom, Ilala Bungoni jijini Dar.

 

Mchezo huo wa kirafiki Global FC kuichakaza DSJ leo Marco Mzumbe, Dar es Salaam unatarajiwa kuwa wa upinzani mkali kutokana na baadhi ya wachezaji wa Global FC kuwahi kusoma katika chuo hicho.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa mmoja ya wachezaji wa Global FC ambaye aliwahi kuwa rais wa chuo hicho, Lunyamadizo Mlyuka alisema: “Hatutakubali kufungwa na wadogo zetu, kama watatufunga basi itakuwa ni fedheha kubwa sana, hivyo tutajitahidi kushinda japokuwa mpira una matokeo ya kikatili,” alisema mchezaji huyo. Katika mechi iliyopita, Global FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kill Veterani.

MAGAZETI AUG 16: KARDIANALI PENGO ANG’ATUKA RASMI


Loading...

Toa comment