Global Habari Dec 01: Waziri Lugola Akanusha Tuhuma Za Kufukuza Wakimbizi

Serikali ya Tanzania imekanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba imekua ikiwafukuza wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika Makambi na Makazi mbalimbali mkoani Kigoma,Tabora na Katavi

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola baada ya Mkutano wa kutiliana saini kati ya pande tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania, Serikali ya Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) lengo ikiwa ni kuwarudisha wakimbizi walioomba kurejea nchini Burundi kwa hiyari yao baada ya amani kurejea nchini humo

 

Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchini Burundi Pascal Barandagiye amesema nchi ya Burundi kuna amani na wanaomba raia wao warejee ili waweze kuijenga nchi yao….

 

Kamishna Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR ,George Okoti Obbo amesema wameshirikiana na nchi mbili za Tanzania na Burundi katika kufikia makubaliano hayo wakiamini Tanzania imekua nchi inayopokea raia wanaopata matatizo katika nchi zao na akiwashukuru raia wa Tanzania kwa ukarimu wao…

 

Serikali za Burundi na Tanzania mnamo mwezi Agosti 2019, ziliingia makubaliano ya kuwarejesha wakimbizi zaidi ya 200,000 kutoka nchini Burundi ambao walikuwa wakiishi hapa nchini. Tanzania inatajwa kuwa nchi pekee inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hivi katibuni takribani wakimbizi 150 kutoa nchini Burundi walisajiliwakatika kambi ya Nyarugusu wilayani kasulu mkoani Kigoma lengo likiwa ni kuwatambua idadi ya wakimbizi waliopo nchini.huku ikitajwa zaidi ya wakimbizi 2000 kutoka Burundi huingia nchini kwa wiki

Toa comment