Global Habari Dec 13 – Vituo Vya Malezi Ya Watoto Vyapewa Siku 14 Kujitathmini
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewapa siku 14 wamiliki wa vituo vya mchana vya malezi ya watoto Mkoani Arusha kurekebisha kasoro zilizopo kabla vituo hivyo havijafungiwa.
Dkt. Jingu ametoa agizo hilo alipotembelea baadhi ya vituo katika jiji la Arusha na kutoridhishwa na uendeshaji wake baada ya kubaini vituo hivyo kutozingatia masharti ya kutoa huduma hiyo ikiwemo maeneo finyu na kuagiza wamiliki wake kutafuta maeneo mengine.

