The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI DEC 15: TANESCO YAELEZA KUIMARIKA KWA UMEME NCHINI

0


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco Dkt Alexandrea Kyaruzi amesema hali ya Upatikanaji wa Umeme nchini imezidi kuimarika huku mfumo wa gridi ya Taifa ukiwa na ziada ukiwa na wastani wa Megawati 200 kwa Siku.

 

Dkt Kyaruzi amesema hadi kufikia Novemba 25 mwaka Huu Mahitaji ya umeme yaliongezeka na kufikia Megawat 1120 ikilinganishwa na mahitaji ya mwaka jana katika kipindi hicho ambayo ilikuwa Megawat 1116.56

Aidha Amewahimiza Wafanyakazi wa Shirika hilo kuongeza jitihada za Ubunifu ili kuhakikisha umeme haukatiki kwenye grade ya Taifa.

 

Mkurugenzi wa Tanesco Dkt Tito Mwinuka na Mratibu wa Umeme Mto Rufiji Mhandisi Steven Manda wakazungumzia Utekelezaji wa Miradi ya Umeme ukiwemo wa Rufiji unaojulikana kama Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere.

 

Mradi huo ambao unafahamika kwa jina la Julius Nyerere, unatazamiwa kuzalisha megawati 2,000 za umeme, hatua ambayo inaelezwa kwamba itasaidia kupunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii.

 

Hatua ya kuanza kwa mradi huo inakuja baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka Mto Rufiji uliofanywa wakati wa utawala wa rais wa kwanza, Mwalimu Julius Nyerere. Ujenzi wa bwawa hilo unaofanywa na wakandarasi kutoka nchini Misri unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 2.9 sawa na shilingi trilioni 6.5 za Kitanzania.

 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Uyole Dk. Tulole Bucheyeki amesema tatizo la Udumavu nchini linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa kama wananchi watatumia njia za kisasa za uzalishaji mazao.

Leave A Reply