The House of Favourite Newspapers

Global Habari Dec 22: Neno La Rais Magufuli Kuelekea Krismas Na Mwaka Mpya

0


Rais Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kusherehekea kwa utulivu sherehe za Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka kuwa na mipango thabiti ya maendeleo kuelekea mwaka 2020.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati wa ibada maalumu Dominika ya nne katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato iliyoongozwa na Padre Henry Mulinganisa, ambapo amepata nafasi ya kuzungumza na wananchi wilayani humo pamoja na watanzania kwa ujumla kuelekea msimu wa sikuu za mwisho wa mwaka.

Waumini wa dini ya Kikristo wanaungana na wakristo wengine duniani katika kusherehekea siku kuu ya Christmass Disemba 25 ya kila mwaka kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mwokozi wao Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Rais Magufuli yuko Wilayani Chato kwa ziara maalumu ya kikazi pamoja na mapumziko ya msimu wa siku kuu ambapo mapema wiki hii amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo Ikiwemo uzenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato, ujenzi wa jengo la ofisi ya Jeshi la Zima moto na Uokoaji, ujenzi wa Msikiti wa kisasa, uzinduzi wa miradi ya visima vya maji katika maeneo ya shule ya msingi Chato.

Leave A Reply