The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 08: Sakata la Mauaji Singida, ACT Wataka Uchunguzi Ufanyike! – VIDEO

Chama cha ACT Wazalendo kimedai kusikitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Singida kuhusu uchunguzi wa Tukio la mauaji linalodaiwa kutekelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Pius Luhende katika kanisa la Adventisti mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho yaliyopo kijitonyama jijini Dar es salaam Katibu wa Itikadi Mawasiliano na Uenezi Ado Shaibu amesema chama hicho kimeshtushwa na taarifa kutoka katika jeshi la polisi mkoani humo iliyonukuliwa na vyomba vya habari.

Aidha Shaibu amesema, kwa mujibu wa Baba wa Marehemu na waumini wa kanisa hilo wamesema aliyemfyatulia risasi marehemu ni Mkurugenzi wa Itigi.

Shaibu amesema chama cha ACT kinalaani tukio hilo la kinyama lililofanyika kwenye nyumba ya Ibada kutaka haki itendeke bila kuangalia cheo cha mtu na mahusiano yake kwa Serikali. February 2 mwaka huu inadaiwa Mfanyabiashara Isaka Petro aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ibadani katika kanisa la Kiadventisti Itigi mkoani Singida na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi Pius Luhende.

Comments are closed.