GLOBAL HABARI FEBR 09: Tamko la Naibu Waziri Masauni kwa Wananchi – VIDEO
Serikali imewataka watanzania kuwa na Umoja bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote ili kulinda amani na utulivu wa nchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifungua Semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwahusisha Viongozi wa Taasisi za Kiislamu lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao.
Akizungumza katika Ufunguzi huo Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum, aliihakikishia serikali kurejea kwa umoja kati ya taasisi mbalimbali za kidini tofauti na utengamano uliokuwepo awali.
Comments are closed.