The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 10: Makamu Rais Atoa Maagizo Mazito Kikao cha Kamati – VIDEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema vikao vya masuala ya Muungano vinapaswa kuzingatia mambo mengi ikiwemo sheria na katiba ili kuenda sambamba na misingi ya muungano iliyowekwa na waasisi wa Taifa.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili masuala ya Muungano katika ukumbi wa Kambarage, Jengo la Hazina jijini Dodoma. Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.

William Lukuvi amekabidhi kiwanja chenye ukubwa wa hekari 30 kilichopo kwenye eneo la mji wa Serikali Dodoma kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bila gharama yeyote kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kimehudhuriwa na Mawaziri wa Serikali zote mbili pamoja na Makatibu Wakuu na Timu ya wataalamu.

Comments are closed.