GLOBAL HABARI FEBR 16: SONGWE YATAJWA KUWA KITOVU CHA UWEKEZAJI SADC -VIDEO
Serikali imeahidi kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara ili kuvutia uwekezaji kwenye Mkoa wa Songwe ambao unatajwa kuwa kitovu cha biashara kwa nchi wanachama wa jumuiya ya SADC.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwekezaji nchini Angela Kairuki wakati akizindua kongamano maalumu la uwekezaji mkoa wa Songwe lililobeba kauli mbiu Songwe ni Lango kuu la SADC,tuwekeze katika viwanda vikubwa,vya kati na vidogo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe David Kafulila amebainisha fursa za uwekezaji kwenye Mkoa wa Songwe huku akibainisha kuwa asilimia 70 ya mizigo ianyotoka kwenye bandari ya Dar es Salaam inapita kwenye mkoa wa Songwe.
Mkoa wa Songwe unatajwa kuwa kiungo muhimu kwenye sekta ya uwekezaji katika kuunganisha Tanzania na baadhi ya nchi wanchama wa jumuiya ya SADC yenye watu takribani milioni 400 na uchumi wa zaidi ya Dola bilioni 600.