The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 26: JPM Akutana na Daktari Bingwa wa UPASUAJI – VIDEO

Rais Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo Ikulu Jijini Dar Es Salaam naDaktari Bingwa wa Upasuaji Wa Ubongo Na Mishipa Ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali Ya Kimataifa Ya Chuo Kikuu Cha Peking Cha Beijing nchini China

Katika mazungumzo hayo rais magufuli ameishukuru Hospitali Ya Kimataifa Ya Chuo Kikuu Cha Peking kwa kukubali ombi la kuanza ushirikiano na MOI huku akimuhakikishia kuwa serikali iko tayari kutoa ushirikiano zaidi kwa kuiimarisha hispotal ya MOI.

Aidha Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa na taarifa za kufanyika kwa mafanikio ya upasuaji wa kwanza uliofanywa na Prof Zhao siku ya jana huku akiamini kuwa madaktari zaidi kutoka peking wataendelea kuja hapa nchini kwaajili yakutoa huduma na mafunzo.

Pia Prof Zhao amemshukuru rais Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha MOI inaimarishwa pamoja na kuweka uwekezaji mkubwa katika miundombinu huku akimuakikishia kuwa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya peking na wizara ya afya hapa nchini yanatekelezwa kikamilifu.

Akizungumzia ujio wa Daktari huyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa rais Magufuli ndiye aliyeelekeza uwepo wa Daktari huyo hivyo wizara ikafanya juhudi za kumleta hapa nchini.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema kuwa serikali imetoa billion 12.5 kwaajili yakuimarisha miundombinu ya hospital ya MOI ili kutoa matibabu yakibingwa ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa watanzania.

 

Comments are closed.