The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI: HUKUMU YA SCROPION YAMTOA MACHOZI SAID

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za kibongo, Salum Njwete maarufu Scorpion miaka 7 jela kwa kosa la kumjeruhi na kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho.

Mahakama hiyo pia imempiga faini ya shilingi Milioni 30 Mtuhumiwa huyo kama fidia kwa kosa la kumjeruhi kwa ajili ya fidia kwa majeruhi huyo.

Akizungumzia hukumu hiyo, mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni majeruhi, Said Mrisho amedai kuwa adhabu aliyopewa Scorpion haitoshi ikilinganishwa na kosa alilotenda huku akieleza kuwa atakwenda kwa Rais Dkt. John Magufuli kumueleza masikitiko yake.

Comments are closed.