The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI JAN 03: ZITTO Kumburuza Mwanasheria Mkuu Mahakamani! – VIDEO

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, pamoja na viongozi wengine wa vyama vya upinzani wamefungua kesi kuhusu muswada uliopelekwa bungeni juu ya sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na bunge kwa minajiRi ya kuupitisha kuwa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Katika mkutano wake Zitto na vyama vingine vya upinzani wamethibitisha kuwa wamefungua kesi katika Mahakama kuu ya Tanzania kwa ajili ya kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge.

Zitto amesema kuwa wamefungua kesi hiyo chini ya hati ya dharura huku wakiomba mahakama kuu kutamka kuwa mswada unaokusudiwa kusomwa bungeni katika mkutano ujao wa bunge mwaka 2019 kuwa ni mswada unaopingana na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake.

Aidha Zitto ameeleza ingawa waliouleta muswada huo bungeni na kusema unaboresha sheria iliyopo ya sasa ya vyama vya siasa, unapinga na kufifisha demokrasia kwa kiasi kikubwa. kesi hiyo imefunguliwa tarehe 20/12/2018 huku wakimlalamikia mwanasheria mkuu wa serikali na kusajili kesi iliyopangwa kutajwa kwa mara ya kwanza tarehe 4/1/2019 mbele ya jopo la majaji.

 

Comments are closed.