The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI JAN 12: Uchumi wa ZANZIBAR Unakua kwa Asilimia 7.7 – VIDEO

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, leo Januari 12 ameongoza wananchi wa Zanzibar katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, na kusema kuwa uchumi wa Zanzibar umekua kwa asilimia 7.7 huku mfumuko wa bei ukithibitiwa kwa tarakimu moja.

Rais Shein ameyasema hayo katika maadhimisho ya miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar yaliyobebwa na kauli mbiu ya Mapinduzi yetu ndiyo umoja wetu, Tuyalinde kwa maendeleo yetu,ambapo amebainisha maendeleo yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 55 ikiwa ni ukuaji wa uchumi,miundo mbinu na upatikanaji wa elimu bure.

Aidha Dkt.Shein ameeleza mikakati ya Serikali katika kuboresha huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuwapatia wananchi huduma ya afya bure kwa kuzingatia sera mpya ya afya ya mwaka 2014.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais, Balozi Seif Ally Iddy, ameipongeza kamati ya maandalizi ya sherehe hizo zilizoenda sambamba na uzinduzi wa miradi ya maendeleo ,matamasha ya burudani na maonyesho ya gwaride toka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.

Comments are closed.