The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI JAN 20: KIMENUKA ! Wafanyakazi 300 Waandamana! – VIDEO

Wafanyakazi zaidi ya 300 wa kiwanda cha Ngomeni Kamba kinachomilikiwa na kampuni ya Katani LTD kilichopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga kinachojishughulisha na uzalishaji wa kamba (TANCORD) wameandama kiwandani hapo wakidai mishahara yao ya miezi mitatu iliyopita sanjari na kutoingiziwa fedha zao NSSF.

Kufuatia adha hiyo wafanyakazi hao walimuomba Rais Magufuli kuingilia kati swala hilo kwani yeye ni mtetezi wa wanyonge ambao dhamira yao ni kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafikiwa na wanafanya kazi kama sera yake inavyosema kuwa hapa kazi tu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TPAWU Geofrey Mgorigo anikiri kuwepo kwa madai hayo na kusema kuwa kwa mujibu wa taarifa alizozipata chanzo ni kutokana na kuyumba kwa uchumi wa kampuni hiyo ambapo amesema hatma ya jambo hilo wameichia kampuni ili ijue nini cha kufanya kwani kumekuwa na ahadi za kila mara zisizotekelezeka.

Mara baada ya waandishi wa habari kufika ofisini kwajili ya kuonana na uongozi baadhi ya viongozi akiwemo Meneja mwajiri Mwaita Kinanda pamoja na Mkurugenzi muendeshaji Damson Mselela waliokuwepo ofisini hapo walikimbia na kujifungia ndani ambapo baada ya kusikia kelele nyingi kutoka kwa wafanyakazi hao iliwalazimu wao kufungua milango na hatimaye kuzungumza.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.