Global Habari Jan 26: Serikali Kuimarisha Udhibiti Wa Rasilimali Madini – Video
Serikali imedhamiria kuwa na mikakati endelevu ya kusimamia na kudhibiti rasilimali madini ili ilete tija iliyokusudiwa kwa Taifa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Jijini Dodoma alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu usimamizi na udhibiti wa rasilimali madini.