Global Habari Jan 28: Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho -Video
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo January 28, 2020 amepokea hati za utambulisho wa Ubalozi kutoka kwa Mabalozi wateule tisa (9) walioteuliwa kuziwakilisha Nchi zao hapa Nchini.
Rais Magufuli amepokea hati hizo Ikulu jijini Dar ambapo miongoni mwa waliowasilisha hati zao ni Maria Amelia Mario De Paiva ambaye ni Balozi wa Ureno nchini, Douglas Foo Peow Yong ambaye ni Balozi wa Singapore nchini na Balozi wa Ufilipino nchini, Alex G. Chua.