The House of Favourite Newspapers

Global Habari Jan 30: Tamko La Serikali Kuhusu Nida, Waziri Mkuu Azungumza -Video

0

Katika kuhakikisha watanzania wote wanapata vitambulisho vya Taifa kwa wakati, Serikali imeongeza idadi ya watumishi kwenye ngazi za Halmashauri ili kuwezesha kufika kwenye vitongoji hadi vijijini kwaajili ya kutoa huduma hiyo.

Hayo yamesemwa na waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anapata kitambulisho hicho.

 

Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa serikali imeongeza jitihada katika kuhakikisha Mtu yeyote ambaye si Mtanzania Hapewi Kitambulisho cha uraia wa Tanzania.

 

Leave A Reply