The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI: KIMBEMBE! MAWAZIRI 5 WA JPM WAVAMIA BANDARI


GLOBAL HABARI: KIMBEMBE! MAWAZIRI 5 WA JPM WAVAMIA BANDARI Mawaziri watano wa serikali ya awamu ya tano wamefanya ziara ya kustukiza katika bandari ya Dar es salaam na kubaini uwepo wa usimamizi mdogo wa shughuli za upakuaji na ukaguzi wa mafuta yanayoagizwa kutoka nje ya nchi.

 

Mawaziri hao ni pamoja na waziri fedha Dkt Philip Mpango, waziri wa Ujenzi Prof Makame Mbarawa, Waziri wa Viwanda Charles Mwijage, Waziri wa Maji Mhandisi Isack Kamwelwe na waziri wa Nishati Dkt Medard Kaleman.

 

Wakizungumza mara badaa ziara hiyo mawaziri hao wametoa maagizo mbalimbali kwa wasimamizi wa vitengo vya udhibiti wa uingiaji wa mafuta katika bandari ya Dar es salaam. Ziara hiyo ya mawaziri hao imekuwa ni muendelezo wa ziara kama hizo ambazo mara kwa mara zimebaini uzembe ama amapungufu katika usimamizi wa shughuli za bandari ya dar es salaam. Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi

Comments are closed.