The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI MACHI 17: Maamuzi Magumu ya Waziri Mbarawa Kuhusu Maji!! – VIDEO

BAADA ya kubaini kuwa Mabilioni ya shilingi yanayotolewa na Serikali kwenye miradi ya maji vijijini yanateketea,huku wananchi wakiwa hawapati maji kutokana na usimamizi mbovu wa Wahandisi wa Halmashauri, serikali imeamua kuanzisha Mamlaka za Maji Vijijini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo .

Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa anasema haya akiwa mkoani Mbeya, akiwa ameanza ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi mbalimbali ya maji, ambapo anasema Serikali imeanzisha utaratibu huo baada ya kubaini kuwa fedha nyingi zinatolewa kwaajili ya miradi ya maji vijijini hazileti tija, kutoka na miundombinu yake kutosimamia kwa uadilifu na hivyo wananchi kutopata maji.

Aidha Waziri wa Maji Profesa Mbarawa amezungumza na watumishi wa Bonde la Ziwa Rukwa pamoja na wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira, na kuhoji sabababu ya mapato kushuka lakini pia akionya kuwa Wizara haitatoa fedha za miradi midogo midogo.

Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya Bashiru Madodi amemweleza Waziri hujuma zinazofanywa na baadhi ya watendaji nyakati za uchaguzi.

Awali Waziri Mbarawa ametembelewa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA Kanda ya Nyanda za juu Kusini na kupokea taarifa.

Comments are closed.