The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI MACHI 19: ZITTO Ampa KAZI Nzito MAALIM SEIF, LIPUMBA Atuma Salamu! – VIDEO

Aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amepokelewa rasmi leo March 19 katika chama cha ACT Wazalendo na kiongozi wa chama hicho Zitto Zuberi Kabwe.

Ni shamrashamra za wanachama wapya waliokaribishwa katika chama cha ACT wazalendo kutoka chama cha wananchi CUF ambao wameambatana na Maalim seif Sharif Hamad katika ofisi za makao makuu ya ACT yaliyopo Kijitonyama Dar es salaam ambapo baada ya kupokelewa kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe akapata wasaa wa kuzungumza na waandishi wa habari.

Hata hivyo Zito alimkabidhi Maalim kadi ya uanachama wa chama cha ACT wazalendo pamoja na viongozi wengine waandamizi waliokuwa chama cha CUF.

Baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama Maalim Seif akapata nafasi ya kuzungumza huku akiwashukuru viongozi wa chama hicho kwa kumpokea yeye pamoja na wanachama wengine na kuahidi kushirikiana katika kukijenga chama.

Huku hayo yakijiri Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba amezungumza na waandishi wa habari na kusema, kwa sasa ni muda wa kukijenga chama na si muda tena wa malumbano.

March 17 mwaka huu Maalim Seif Sharif Hamad alitangaza kujiondoa katika chama cha CUF baada ya mahakama kuamua uhalali wa mweyekiti wa CUF Profesa Lipumba ambaye anatambuliwa na Msajili wa vyama vya siasa.

Comments are closed.