The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI MACHI 26: RPC Asimulia WALIVYOUA Majambazi 5, Wakakamata Silaha – VIDEO

Jeshi la polisi mkoani Kigoma limefanikiwa kuwauwa majambazi watano waliokuwa wakijiandaa kutekeleza tukio la utekaji magari katika eneo la pori la kijiji cha Rusohoko

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa walipokea taarifa ya mipango ya tukio hilo na kufanikiwa kumkamata Jambazi mmoja ambaye walimlazimisha awaoneshe wenzake walipo ambapo baada ya kufika eneo la tukio maajibizano ya risasi yalitokea yaliyosababisha askari wawili kujeruhiwa pamoja na kukamatwa Bunduki mbili za kivita aina ya AK 47,risasi 20 pamoja na magazine mbili zilizokuwa zikitarajiwa kutumiwa kwenye tukio hilo .

Katika tukio jingine jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akujulikanae kwa jina la Osward Zababa mkazi wa Kagerankanda akiwa na risasi 105 za SMG pamoja na magazine moja ambapo wananchi wametoa ombi kwa jeshi hilo kuongeza ulinzi ili kukomesha matukio kama hayo.

Comments are closed.