The House of Favourite Newspapers
gunners X

GLOBAL HABARI: Mbowe Atua Mbeya Kusikiliza Kesi ya Sugu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe, amefika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.

Mbowe akiongozana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Sophia Mwakagenda wamefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ambayo inasikilizwa mfululizo kwa wiki hii yote.

Jana jumanne mahakama hiyo ilikataa kutoa dhamana kwa mbunge huyo na kuamuru arudishwe rumande wakati ushahidi wa kesi yake ukianza kusikilizwa kuanzia hii leo.

Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anakabiliwa na kesi kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya muungano Dkt John Magufuli wakati wa mkutano wake wa hadhara uliofanyika mwishoni mwaka jana. Mwisho.

Comments are closed.