The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI: MBUNGE SUGU ANYIMWA DHAMANA, ARUDISHWA RUMANDE


MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepelekwa mahabusu katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya baada ya kukosa dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili. Sugu na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Januari 16 na kupelekwa mahabusu leo Jumanne Januari 16, baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.

 

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa dhamana. Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya uchochezi kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Desemba 30, mwaka jana akiwa katika viwanja vya mikutano vya shule ya msingi Mwenge iliyopo jijini Mbeya ambapo Sugu anadaiwa kutamka kuwa rais ni muuaji. Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis… TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis… TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari

Comments are closed.