The House of Favourite Newspapers

Global Habari Nov 16: Mwanamke Mmoja Auawa Geita, RPC Aeleza Tukio Zima – Video

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Naomi Mshera mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa kijiji cha Ntinaji Wilayani Geita amekutwa ameuwawa kwa kunyongwa na watu wasio julikana kwenye eneo la shamba la Mahindi.

 

Akizungumza na GLOBAL ONLINE TV ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea Novemba 13 majira ya saa moja usiku wakati mwanamke huyo akitokea kwenye kikao cha ndugu ambapo alikutana na wahalifu hao wanaosadikiwa kumnyonga, kumfunika na kitenge na kisha kumtupa kwenye shamba.

 

Kamanda Mponjoli ameelezea hatua ambazo zimechukuliwa na Jeshi la polisi baada ya kubainika kwa tukio hilo na juhudi za kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

 

Kamanda Mponjolo ameongeza kuwa mazingira ya tukio hilo ni Dhahiri na kuwa tayari Jeshi la Polisi Mkoani Geita linawashikilia watu wawili ambao watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi za kiuchunguzi.

Comments are closed.