The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI NOV 17: KAMPENI za UCHAGUZI ZAANZA Rasmi LEO, Waziri JAFO Athibitisha


Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa kufanya kampeni za kistaarabu zinazolenga kujenga na kuimarisha Amani hapa nchini.

 

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wagombea wa nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa kufanya kampeni za ustaarabu.

 

Aidha Waziri Jafo amewata wanachi kutumia haki yay a msingi kwa kujitokeza kuwasikiliza wagombea hao kwenye mikutano ya kampeni iliyofunguliwa rasmi hii leo ili kujua na kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

 

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ametumia fursa hiyo kutoa onyo kwa wanafunzi wanaoshiriki katika kuhujumu na kuharibu miundombinu ya shule inayojengwa kwa gharama za kodi za wananchi hapa nchini.

Uchaguzi huu unafanyika wakati vyama saba vya upinzani ikiwemo Chadema, CUF, ACT Wazalendo, Chaumma, NLD, UPDP,CCK na NCCR Mageuzi vikiwa vimetangaza kutoshiriki kwa madai ya kukiukwa kwa baadhi ya taratibu za uchaguzi huku vikitoa wito kwa rais wa taifa hilo, John Magufuli kufuta uchaguzi huo.

Comments are closed.