Global Habari Nov 24: Magufuli Akasirishwa Na Mashirika 187, Atoa Siku 60 Tu..
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ametoa siku 60 kwa kampuni, mashirika na taasisi 187 zilizoshindwa kutoa gawio kwa serikali, kutoa kabla ya hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.
Rais Magufuli ametoa uamuzi huo katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati akipokea gawio na michango kutoka taasisi na mashirika ya umma shillingi Trillioni 1.05 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kutoka kampuni ambazo Serikali ina hisa
Aidha rais magufuli ametoa pongezi kwa mamlaka ya mapato nchini (TRA) kwa jitihada kubwa inayofanya ya kukusanya mapato ya kodi nchini, ambapo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ukusanyaji wa mapato ya kodi umeongezeka kutoka wastani wa shillingi billioni 850 hadi kufikia trillioni 1.3 na hapa anafafanua zaidi
Jumla ya Kampuni 79 zimeshiriki kwenye utoaji wa Gawio hilo Ikulu Ndogo ya Chamwino Jijini Dodoma Ambapo jumla ya Trilioni 1.05 zimekusanywa huku Mamlaka ya Bandari Tanzania ikitoa Gawio kubwa la shilingi Bilion 169 likifuatiwa na Mamlaka ya Mwasiliano Tanzania ikitoa Shilingi Bilioni 85.8 na Shirika la Umeme Tanzania Tanesco likitoa Gawio la Shilingi Bilioni 1.4
Comments are closed.