The House of Favourite Newspapers

Global Habari Nov 26: Moto Waua Watoto Watatu Wa Familia Moja Dsm

Watoto watatu wa Familia moja akiwemo Idris Masoud, Ikram Masoud na Abubakari Masoud wamepoteza maisha jijini Dar es salaam baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuungua kwa Moto.

 

Tukio hilo limetokea Novemba 24, 2019 maeneo ya Kimara suka jijini Dar es salaam na baada ya Global Tv kuzungumza na Mama Mzazi wa watoto hao Tatu Bakari amesema kuwa akiwa nje alisikia sauti ya mwanaye aliyekuwemo ndani ya nyumba hiyo akiomba msaada pasipokujua chanzo cha moto huo.

 

Global Tv imepata fursa ya kuzungumza na Ndugu wa Marehemu Ustadhi Yahaya Hemed Nassoro aliyekuwepo msibani hapo, ameelezea namna alivyosikitishwa na Msiba wa ndugu zake.

Comments are closed.