The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI NOV 7: Maamuzi ya serikali kuhusu Ajali za Meli – VIDEO

Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kufuatia ajali za majini zinazopelekea watanzania wengi kupoteza maisha ikiwemo ajali ya MV Nyerere serikali imetunga kanuni na sheria zakusimamia vyombo vya usafiri wa majini ili kuweza kupunguza ajali hizo.

Akijibu swali la mbunge wa Nunge Yusuph Haji Hamis Katika kipindi cha maswali na majibu naibu waziri Nditiye amesema tayari serikali imechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kutatua changamoto zinazotokana na usafiri wa majini.

Katika hatua nyingine naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto dkt faustine Ndungulile akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa viti maalum CHADEMA Susan Lyimo amesema Serikali haijaweka ukomo wa watoto wanaotakiwa kuzaliwa ila wazazi wanatakiwa kuzaa watoto ambao wanaweza kuwalea.

Mkutano wa 13 wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania umeanza jana jijini Dodoma ambapo kikao hicho kinajadili mpango wa maendeleo ya taifa kwa mwaka 2019/2020 kama ulivyowasilishwa na waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango.

 

Comments are closed.