GLOBAL KUJA NA TAMASHA KUBWA LA SHUKRANI

KAMPUNI ya Global Publishers; wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Championi na Spoti Xtra, inatarajia kuwakonga nyoyo mashibiki wa burudani na wasomaji wa magazeti yake katika tamasha bab’ kubwa linalokwenda kwa jina la Shukrani.

 

Tamasha hilo linatarajia kufanyika hivi karibuni kwa kuwakutanisha wasanii kibao wa Bongo Fleva ambao watalishambulia jukwaa la Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Meneja wa Global Publisher, Abdallah Mrisho amesema lengo la kampuni hiyo kuandaa tamasha hilo kwanza ni kuwashukuru wasomaji wa magazeti ya Global ambao wameiunga mkono kampuni kwa takriban miaka 20 lakini pia kuwaweka karibu wasomaji kwa kuwatambulisha promosheni mpya ya pikipiki inayoendelea.

“Kama kampuni tumepanga kuwashukuru wasomaji wetu kwa kutuunga mkono kwa takriban miaka 20 tangu tuanze kuchapisha magazeti. Tumekuwa tukitoa magazeti yetu tofauti kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Tumepanga kuwashukuru lakini pia kuwapa burudani kubwa ya muziki bure kabisa bila kiingilio chochote.

 

“Tuna orodha kubwa ya wasanii watakaolipamba jukwaa siku hiyo ambayo tutaitangaza hivi karibuni. Kikubwa ni wasomaji kuendelea kusoma magazeti yetu kila siku wataipata hiyo fursa bure kabisa.

“Lakini kwa jinsi tunavyowajali wasomaji wetu, sasa hivi tupo kwenye msimu wa kugawa zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki kila wiki. Msomaji kwa kununua gazeti lolote la Global kwa shilingi 800 tu unaweza kujishindia zawadi ya pikipiki,” alisema Mrisho.

 

Kama hiyo haitoshi, Mrisho alisema wasomaji wa magazeti ya Global hawatanufaika tu na pikipiki kila wiki bali wataweza kujipatia zawadi mbalimbali zikiwemo jezi, ada ya shule, dinner sets na t-shirt.

“Tumedhamiria kugawa zawadi nyingi sana kila wiki hivyo wasomaji wetu hawatakuwa tu wanapata habari motomoto kama walivyozoea bali pia watapata zawadi kibao,” alisema Mrisho.


Loading...

Toa comment