The House of Favourite Newspapers

Global Publishers: Tunalaani upotoshaji huu

0

GPL_Logo_FinalWEWB

1

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa wa makusudi unaofanywa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii kwa kugeuza maudhui ya  habari iliyochapishwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda la Januari 26, 2015 iliyokuwa na kichwa cha habari “OFM YAMSHUGHULIKIA WAZIRI WA JK” kwa lengo la kuihadaa jamii iamini kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (enzi hizo alikuwa naibu Tamisemi) alifanya jambo baya hotelini.

Ukweli ni kwamba kitengo chetu cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) kilishughulikia taarifa za vyanzo vya habari kuwa waziri huyo aliingia hotelini huku vyanzo hivyo vikishindwa kujua alikwenda kwa lengo gani? Baada ya uchunguzi wa kina OFM ilibaini kuwa Waziri Majaliwa alikuwa na kikao cha kikazi jambo ambalo OFM ilimpongeza.

Aidha waliosoma habari hiyo kwa kina ndani ya gazeti baada ya kuchapishwa waliipongeza OFM pamoja na Waziri Majaliwa kwa kile kilichofanyika.

Kwa msingi huo tunalaani na kuwaonya wale wote wanaotumia gazeti letu kumchafua Waziri Mkuu-Tutachukua hatua zinazostahili kwa wahusika.

MHARIRI MTENDAJI – GLOBAL PUBLISHERS LTD

Imetolewa: Novemba 20, 2015

Leave A Reply